Thursday, February 02, 2006

Waziri Mkuu Bw. Edward Lowassa, amewataka Watanzania kuiga mfamo wa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP katika utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

Bw. Lowassa amesema miti mingi iliyoko Mkoani Kilimanjaro imetokana na juhudi binafsi za Bw. Mengi. ’Nampongeza sana Bw. Mengi kwa juhudi zake kubwa za kupanda miti. Napenda wananchi wengi kuiga mfano huo’ alisema.

Hivi kumbe kupanda miti ndiko kutunza Mazingira? Mimi nilikuwa Sijui. Kwa hiyo hata kama mtu atakuwa na maelfu ya viwanda vinavyotoa gesi ya kuharibu ozoni atakuwa ametunza Mazingira. Nasikia ziwa Manyara limekauka kwa asilimia 95. Haya huyu Mwenyekiti wa kusimamia mazingira anayesifiwa na waziri Mkuu hakuwepo wakati hilo linaendelea kutokea? Kuna mtu ananinong'oneza hapa eti Uenyekiti wake wa mazingira ni wa kumshughulikia mmiliki wa Karibu Textile tu basi baada ya hapo ni kupozi tu mbele ya kamera

6 Comments:

Blogger Ndesanjo Macha said...

Kuna mitazamo ambayo tunayo kutokana na kushabikia tu. Mojawapo ni suala la mazingira kufanywa kuwa ni upandaji miti peke yake. Karibu viwanda vyote nchini havina teknolojia sahihi ya kutupa au kuharibu taka zake bila kuharibu mazingira. Kuna wakati, nadhani ni Makene, mwanablogu mmoja aliandika kuhusu mifuko ya "rambo." Nchi zenye kujali uhali wa vizazi vijavyo zina sera za kuondoa matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo huwa haiharibiki miaka na miaka. Kati ya sera hizo ni pamoja na kuweka kodi kubwa ili watu wasiinunue, kusamehe kodi kwa kiasi fulani kwa biashara zinazotumia mifuko ya karatasi, n.k. Ukija kwenye suala la magari yanayotoa moshi wa kaboni, nchi hizo zinatumia kila aina ya kampeni kushawishi wananchi wake kutumia baiskeli (ambapo pia ni mazoezi), kutumia usafiri wa umma (ambapo lazima usafiri huo uimarishwe kwa mipango kabambe), kushawishi watu kutumia gari moja (kwa mfano kama wewe na jirani yako mnafanya kazi ofisi moja, kwanini kila mmoja aendeshe gari wakati mnaweza kutumia moja? Au unahofu watu hawataona kuwa nawe una gari?), kuwekeza kwenye taknolojia za kubadili taka kuweza kutumiwa tena kwa namna moja au nyingine, kufundisha wananchi juu ya matumizi bora ya maji (kwa kuwa kuna watu wanadhani tukiendelea kutumia maji tunavyotumia leo bado yataendelea kuwepo daima. Kuna vyoo, kwa mfano, siku hizi ambavyo havitumii maji kabisa.)

Utashangaa huyo Mengi wakati akienda kazini anapita kwenye mitaa ambayo mabomba ya maji hupasuka mara kwa mara kisha kuzibwa kwa kutumia mpira wa manati lakini anaweza asione hilo kuwa lina uhusiano na mazingira.

Majuzi Michuzi alituwekea picha ya Tabata ilivyo siku hizi. Watu huwa wananiambia, "Tabata imejengeka kweli. Huwezi kuamini kuwa ilikuwa pori." Mimi sioni kama kitendo cha kukata miti na kujenga majumba ya kukaa, baa, gereji, n.k. ni suala la kujivunia. Siku hizi kuna wahandishi na wana mipango miji ambao wanatumia mbinu za ujenzi na upanuzi wa miji bila kufanya makosa tunayofanya ya kukata miti kwa kudhani kuwa "pori" ni alama ya kuwa nyuma kimaendeleo na majengo katika jangwa la kujitakia ni maendeleo.
Tazama picha ya blogu murua ya Michuzi: http://issamichuzi.blogspot.com/2006_02_01_issamichuzi_archive.html

Picha yenyewe shuka chini karibu na mwisho wa ukurasa.

1:37 PM  
Blogger John Mwaipopo said...

Bwana Mengi ni mtaalamu wa kujua nini kitamuongezea pato katika biashara zake. Aliibuka na mazingira wakati dunia ilipokuwa imehadaiwa na sera za mazingira hasa baada yamkutano wa mwaka 1991 kule Rio De Jeneiro, Brazil. Halafu akajiingiza kwenye Ukimwi baada ya dunia kuanza kuongelea suala hilo akijua si haba. Sasa amejitumbukiza kwenye matatizo ya ugonjwa wa moyo akitaraji jambo. Mimi sikujua kuwa kabla Mengi hajazaliwa Moshi ilikuwa Jangwa!

12:51 PM  
Blogger John Mwaipopo said...

Wewe Mustafa unatafutwa hapa kibarazani. Umetoweka kimyakimya. Kulikoni?

3:47 PM  
Blogger Rama Msangi said...

Huu ndio upuuzi ambao kila kukicha tunaufanya...kila uchao utasikia kampeni za kupanda miti zimezinduliwa sehemu fulani, viongozi wakubwa wakubwa (sio wakuu msininukuu vibaya) nao utaona wako mbele ya kamera wanazindua kampeni za kupanda miti tena kando kabisa ya kijito kinachotiririsha kemikali za kutoka kwenye kiwanda cha Muezekaji... ah samani Muwekezaji toka nje ya nji hii.....si kwamba hajui kuwa hautakua, bali sasa atafanyaje wakati anataka na msimu ujao wa uzinduzi apate vielelezo vya wahisani kuongeza hela za kampeni hiyo?? Tunacheza tu na roho zetu

6:37 AM  
Blogger zarena kewat said...

That's what everyone likes. You have a good imagination. Great post thanks you
vimax canada

9:36 AM  
Blogger myslot said...

ไม่ต้องออกบ้านก็สามารถดูหนังได้ ดูหนังออนไลนื Captain Marvel กัปตัน มาร์เวล (2019) คุณต้องลองเลย หนังใหม่

https://www.doonung1234.com/

2:59 AM  

Post a Comment

<< Home