Monday, January 30, 2006

Mambo hayo! eti Supika wa bunge anadai kuwa wabunge wa Tanzania ndio wanaolipwa kidogo kuliko wote katika nchi za 'komoni " wealth. Sasa sijui anajua walimu wa tanzania, madaktari katika hiyo komoni wealth wanalipwaje? Ingekuwa vyema pia akajua ni kiasi gani watanzania tunakipata katika mikataba ya madini ikilinganishwa na nchi nyingine za komoni Weath, bei ya umeme je ikoje ukilinganisha na mahayo komoni weath. Halafu naomba nikumbusheni Eti Komoni wezi ndio kitu gani? na kinamuhusu vipi mpiga kura wa kule Igunga tabora?

5 Comments:

Blogger Ndesanjo Macha said...

Anachosema spika ni matusi makubwa kwa watanzania wanaomaliza mshahara wao tarehe sita ya mwezi, mshahara unaopaswa kuwasukuma hadi mwisho wa mwezi. Kwani wakilipwa hela kidogo ukilinganisha na wengine kwenye nchi nyingine ndio nini? Hatuwalinganishi na wabunge wengine bali tunalinganisha kipato chao na kipato cha watanzania wengine. Toka tupate uhuru mishahara ya walimu tunaambiwa kuwa "inashughulikiwa."
kwanza tuifanyie utafiti hii kauli yake, inawezekana kuwa sio kweli kuwa wao ndio wanalipwa kidogo maana wamezoea kutudanganya maana wanajua tutawaamini. Lakini hata kama ni kweli bado hiyo sio hoja ya kuridhisha.

4:37 AM  
Blogger Ibrahim M. Bwire said...

wana marupurupu kiasi gani?
ni wafanyakazi gani wanaokopeshwa magari, na kupata posho ya utumishi mwema baada ya miaka mitano ya utumishi wao? tena wakati mwingine majimboni hakuna walichofanya.

labda mwenye nacho huongezewa? tusemeje?

7:56 AM  
Blogger FOSEWERD Initiatives said...

naumgana na watoa hoja na hasa ndesanjo ambaye amesema haya ni matusi makubwa!!!! ni kweli ni makubwa!!! ndio maana ndesanjo wimbo wa taifa unamtia kichefuchefu pale unapofika wabariki viongozi wake!!!

ni matusi makubwa...elimu inashuka, wataalamu wanakimbia kwenda kwenye vinchi vilipata uhuru baada yetu...wachilia mbali za madola kwa ujumla maana wengi wametuzidi...na waheshimiwa ndio wanaona raha kuongoza mawe badala ya watu (hawahojiwi - wanashusha neti)...ukisikia mtu anakimbilia msumbiji au zambia si kasheshe kweli?

8:12 AM  
Blogger John Mwaipopo said...

Mustafa hebu niandikie at johnmwaipopo@yahoo.com nikukumbuke vema. Yaonyesha wanifahamu fika weye

10:42 AM  
Blogger zarena kewat said...

That's what everyone likes. You have a good imagination. Great post thanks you
vimax canada

9:38 AM  

Post a Comment

<< Home