Monday, January 30, 2006

Hivi mnamkumbuka Reginald Mengi? Mtu ambaye kila siku anawaasa watanzania waondokane na umasikini wa fikra ili nao wawe tajiri kama yeye. Hivi mnafahamu jinsi wafanyakazi wake katika makampuni anazomoliki wanavyokuwa matajiri kwa sababu bosi wao anataka kuwa tajairi? mnafahamu jinsi anavyowapenda walemavu kiasi kwamba huwakaribisha kula nae chakula na kucheza nae Twanga pepeta? Mtu huyu safi eeeenh?

5 Comments:

Blogger FOSEWERD Initiatives said...

sikujua kuwa pia anatajirisha wafanyakazi wake pia. mwendo mzuri charity srarts at home!

8:13 AM  
Blogger must said...

Mimi sijasema kama anatajirisha wafanyakazi wake bali nimetoa changamoto kumfuatilia undani wake.

5:02 AM  
Blogger boniphace said...

Mustapha acha utani hilo la kutajirisha wafanyakazi lifafanue. Maana naujua ukweli wa Media za Tanzania na kuhusu Media zinazolipa kwa kubangaiza. Sisemi sasa nataka kwanza ufafanuzi wako.

11:11 AM  
Blogger Ndesanjo Macha said...

Unajua Mengi ananikumbusha wafanyabiashara Waislamu wa pale Dasalama. Kuna wafanyabiashara wanaojifanya wacha mungu, kila ijumaa wanagawa fedha kwa watu masikini...hasa mitaa ya kariakoo. Lakini wafanyabiashara hao hao "wanaosaidia" masikini kila ijumaa ili kupata thawabu wanakandamiza wafanyakazi wao, wanafanyisha kazi kupita kiasi, wanawapunja mshahara, n.k. Kwakuwa kumlipa mfanyakazi wako sio tena halikufanyi uonekane mbele ya watu kuwa wewe ni "mtu wa mungu" wafanyabiashara hawa hawatumii ucha mungu wao kulipa ujira halali wafanyakazi wao. Ucha mungu wao ni kutoa vishilingi kadhaa kwa masikini. Tendo hili tofauti na lile la mshahara linaonekana na watu na linawafanya waamini kuwa wanafanya tendo la kidini. Unafiki wahedi!

Sasa Mengi kama anatajirisha wafanyakazi wake atakuwa ameanza karibuni maana kwa miaka mingi wafanyakazi wake wamekuwa wakilalamika kichinichini. Na labda basi sio wafanyakazi wote maana najua wafanyakazi wake wanaolalamika hadi leo. Najua pia waandishi wa kujitegemea kwenye magazeti yake wanaolalama njaa.

Kula na walemavu ndio mtindo huo huo wa kutoa vishilingi siku ya ijumaa. Au kutoa mamilioni kanisani huku jirani yako au wafanyakazi wako wakiwa hawajiwezi kwa ufukara.

Anakula na walemavu kisha anapigwa picha na habari zinajaa kwenye vyombo vyake vyote vya habari...

8:54 PM  
Blogger must said...

Kaka Ndesanjo asante kwa kufufua mjadala kwa upandea mwingine wa shilingi, wewe ni mtu 'mwoga' unayeogopa kesho tanzania utakuwaje kama hali ikiendelea hivi kama ambavyo Jenerali ulimwengu amekuwa akiogopa siku zote. Watu majasiri kama Makene hawaogopi wao ,wanafikiria kesho watatembeleaje na benzi na kuwatesa classmate zao walio wahi kusoma nao. Boni anajua fika Media za Bongo na unamjua vizuri Mengi sasa anaogopa nini kusema? Hata mafukara hutajirishwa ufakara. Kwani maana ya utajiri ni nini? Si ukwasi wa kitu? kama ukiwa na ukwadsi katika ufukara wewe si umetajirishwa huo ufukara ulionao?

5:13 AM  

Post a Comment

<< Home